Return to Index

106

107

Ewe Baba wa Mbinguni

108
SongInstrumental
	

1. Ewe, Baba wa Mbinguni, Usikie twombalo Hapa chini duniani, Na uwe radhi nalo Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! 2. Watu hawa mbele zako, Na mbele ya kanisa; Watimize Neno lako Wanakutana sasa. 3. Kama Yesu na Kanisa, Ni mmoja, na hivyo, Watu hawawape sasa Wawe mmoja vivyo 4. Walinde, Bwana, daima, Wabariki nyumbani Uwape nyingi salama Humu ulimwenguni. 5. Wabariki, ewe Bwana, Watu hawa wawili, Wape upaji wa wana, Wafurahishwe kweli. 6. Siku za duniani Zitakapopungua, Wape kurithi Mbinguni Mema ya kwendelea.