Return to Index

127

128

Mmoja apita wote

129
SongInstrumental
	

1. Mmoja apita wote, Atupenda; Zaidi ya ndugu wote, Atupenda; Rafiki wa duniani, Wote hatuwaamini; Yesu kwa kila zamani, Atupenda. 2. Kumjua ni uzima, Atupenda; Jinsi ajaavyo wema Atupenda; Yeye ametununua Kwa damu aliyomwaga, Dhambini kutuokoa, Atupenda. 3. Sasa tunaye rafiki, Atupenda; Hupenda kutubariki; Atupenda; Twapenda kumsikia, Atwita kukaribia, Nasi tutamwamania, Atupenda. 4. Husamehe Dhambi zetu, Atupenda; Hushinda adui zetu, Atupenda; Anatwonea huruma, Hatupati ila mema, Anatwongoza salama, Atupenda.