Return to Index

20

21

Roho yangu hima na taa

22
SongInstrumental
	

1. Roho yangu hima, na taa yako Kaiwashe vyema, hapa si pako; Nguvu zote pia za duniani Hazitakudhuru ukiamini. Yesu yuko mbele, Yesu yu nyuma, Yesu vivyo kando, walindwa vyema. 2. Adui shetani, na nguvu zake, Bwana ameshinda, kwa kifo chake; Wewe nguvu huna, huna kabisa, Ndiwe mpungufu, mnyonge hasa. 3. Toka na mapema, mbele ya wote, Omba, bisha sana, maisha yote; Vita vikaliko, macho ukae, Jivike silaha, nawe sishindwe. 4. Bwana Yesu ndiye kwako mchunga, Neno lake Bwana ndilo upanga; Mbingu zitakwisha, na nchi pia, Neno lake Bwana laendelea.