Return to Index

22

23

Nionapo amani kama shwari

24
SongInstrumental
	

1. Nionapo amani kama shwari, Ama nionapo shida; Kwa mambo yote umenijulisha, Ni salama rohoni mwangu. Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu. 2. Ingawa shetani atanitesa, Nitajipa moyo kwani Kristo ameona unyonge wangu, Amekufa kwa roho yangu. 3. Dhambi zangu zote, wala si nusu, Zimewekwa msalabani; Wala sichukui laana yake, Ni salama rohoni mwangu. 4. Ee Bwana himiza siku ya kuja, Panda itakapolia; Utakaposhuka sitaogopa Ni salama rohoni mwangu.