Return to Index

36

37

Waitwa mwovu na Bwana

38
SongInstrumental
	

1. Waitwa, mwovu, na Bwana Umwendee hima sana, Usafiwe dhambi zako, Humwoni ni mwema kwako? Unaitwa! Itika tu! Umwendee Bwana Yesu! Sifiche makosa yako, Uungame dhambi zako! Kristo tu umuamini, Ndiyo njia ua Mbinguni. 2. Alilipa damu yake Ili kukukweza kwake; Alikufa yeye Bwana, Mimi nawe tuwe wema. 3. Ukifanywa kuwa mwema Mwishoni utasimama, Utaingia rahani Na wapenzi wa zamani. 4. Ni mwanga tu, nchi ile; Uovu hauko kule, Kwamba wataka ufike Sharti huku uosheke.