Return to Index

62

63

Ndugu wa kirohoni

64
SongInstrumental
	

1. Ndugu wa kirohoni Mliokombolewa, Tafakarini sana Yatupasayo. Wapenzi wake Yesu Tuliokombolewa Tujitoe kabisa Wengi waponywe. 2. Siku itatimia Tutakapoulizwa Wale wa nyumba zetu Na majirani 3. Tujitoeni, ndugu, Tukahubiri Injili. Atutumie Roho kuponya wengi. 4. Wasiokombolewa Ni wengi vijijini, Wataokolewaje Tukiogopa? 5. Bwana alijitoa Akapotewa mengi, Ili atuokoe, Tusiwe waoga. 6. Aliyetununua, Kwa kuimwaga damu, Angalieni sana Msimwepuke.