Return to Index

67

68

Mungu msaada wetu

69
SongInstrumental
	

1. Mungu msaada wetu Tangu myaka yote, Ndiwe tumaini letu La zamani zote. 2. Kivuli cha kiti chako Ndiyo ngome yetu. Watosha mkono wako Ni ulinzi wetu. 3. Kwanza havijakuwako Nchi na milima, Ndiwe Mungu; chini yako Twakaa salama. 4. Na myaka elfu ni kama Siku moja kwako; Utanilinda daima Tu wenyeji wako. 5. Binadamu huondoka, Mwisho hana kitu; Kama ndoto hutoweka Ndivyo hali yetu. 6. Ila wewe Mungu wetu Ndiwe wa kudumu; Ndiwe bora, ngome yetu Twakaa dawamu.