Return to Index

78

79

Msalaba wa aibu

80
SongInstrumental
	

1. Msalaba wa aibu, Ulinipa amani; Uliniondoa kifungoni, Nilimotesekea. 2. Ee, Mwokozi wangu, Yesu Nitamwendea nani? Najiweka msalabani, Nikaoshwe damuni. 3. Nakupenda Bwana Yesu, Kwa kunipenda kwako, Napendezwa nikutumikie Maisha yangu yote. 4. Usifiwe Bwana Yesu, Kwa ulivyonifia, Aleluya, nakushukuru, Uliyenikomboa. 5. Msalaba ulishinda Nguvu zake adui, Ili mimi nikombolewe, Niwe mwana wa Mungu.