Return to Index

93

94

Siku ya Mbinguni kujawa na

95
SongInstrumental
	

1. Siku ya Mbinguni kujawa na sifa, Dhambi zilizidi duniani; Yesu akaja azaliwe mtu, Awe na watu ulimwenguni. Alinipenda, alinifia, Ameondoa na dhambi zangu; Alifufuka nipewe haki, Yuaja tena Mwokozi wangu. 2. Na siku moja walikwenda naye, Wakamkaza msalabani; Aliumia, aliaibishwa, Ili atuokoe dhambini. 3. Siku hiyo wakamlaza chini Kaburini alipumzika; Matumaini yetu wenye dhambi, Ni mwokozi, kwake twaokoka. 4. Kaburi likashindwa kumshika; Jiwe likatoka mlangoni, Alifufuka kwa kushinda kwake, Naye yuko milele Mbinguni. 5. Siku moja atatujia tena; Utukufu wake tutaona; Atawaleta na wapenzi wetu; Mwokozi: wangu, tutaonana.