Return to Index

101

102

Kazi yangu ikiisha nami nikiokoka;

103
SongInstrumental
	

1. Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka; Na kuvaa kutokuharibika, Nitamjua Mwokozi nifikapo ng’amboni; Atakuwa wa kwanza kunilaki. Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso; Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari. 2. Furaha nitapata nikiona makao Bwana aliyotuandalia; Nitamsifu mwokozi kwa rehema na pendo Vilivyonipa pahali Mbinguni. 3. Nao waliokufa katika Bwana Yesu, Nitawaona tena huko juu; Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni, Nataka kumwona Mwokozi kwanza. 4. Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha, Pasipo machozi wala huzuni. Nitauimba wimbo wa milele; lakini Nataka kumwona Mwokozi kwanza.