Return to Index

102

103

Kaa nami ni usiku tena;

104
SongInstrumental
	

1. Kaa nami, ni usiku tena; Usiniache gizani, Bwana; Msaada wako haukomi; Nili peke yangu, kaa nami. 2. Siku zetu hazikawi kwisha, Sioni la kunifurahisha; Hakuna ambacho hakikomi, Usiye na mwisho kaa nami. 3. Nina haja nawe kila saa; Sina mwingine wa kunifaa; Mimi nitaongozwa na nani Ila wewe? Bwana, kaa nami. 4. Sichi neno uwapo karibu; Nipatalo lote, si taabu; Kifo na kaburi haviumi; Nitashinda kwako, kaa nami. 5. Nilalapo nikuone wewe, Gizani mote nimulikiwe; Nuru za mbinguni hazikomi, Siku zangu zote kaa nami.