Return to Index

103

104

Twasoma ni njema sana

105
SongInstrumental
	

1. Twasoma, ni njema sana Mbinguni, kwa Bwana; Twasoma, dhambi hapana, Mbinguni kwa Bwana; Malaika wema wako, Vinanda vizuri viko, Na majumba tele yako, Mbinguni kwa Bwana. 2. Siku zote ni mchana, Ni nchi ya raha; Wala machozi hapana, Ni nchi ya raha; Walioko wanuona Uso wa Mwokozi, tena Jua jingine hapana, Ni nchi ya raha. 3. Nyama na vitu viovu Havimo kabisa; Kifo nacho, na ubovu, Havimo kabisa. Ni watakatifu wote, Wameoshwa dhambi zote; Wasiosafiwa wote Hawamo kabisa. 4. Tuna dhambi, pia sote, Mwokozi akafa; Kwake tutaoshwa zote, Mwokozi akafa; Kwake twapata wokovu, Tutawona utukufu; Mbinguni tutamsifu; Mwokozi akafa. 5. Baba, mama, ndugu zetu, Twendeni kwa Bwana; Huku chini sio kwetu, Twendeni kwa Bwana; Tusishikwe na dunia, Na dhambi kutulemea; Tutupe vya chini pia, Twendeni kwa Bwana.