Return to Index

108

109

Nitaimba ya Yesu

110
SongInstrumental
	

1. Nitaimba ya Yesu, Kwa rehema zake, Baraka nyingi sana Nimepata kwake; Nitaimba ya Yesu, Sadaka ya Mungu, Alimwaga damu Ukombozi wangu. 2. Nitaimba ya Yesu Hapa siku zote, Nitakapokumbuka Vyema vyake vyote; Nitaimba ya Yesu Hata mashakani, Yeye atanilinda Mwake ubavuni. 3. Nitaimba ya Yesu Niwapo Njiani; Takaza Mwendo, hata Nifike Mbinguni; Nikiisha ingia Mlangoni mle, Yesu nitamwimbia Mbinguni milele.