Return to Index

109

110

Mapya ni mapenzi hayo

111
SongInstrumental
	

1. Mapya ni mapenzi hayo, Asubuhi tunayo, Saa za giza hulindwa Kwa uzima kuamshwa. 2. Kila siku, Mapya pia Rehema, wema, na afya, Wokofu, na msamaha, Mawazo mema, furaha. 3. Tukijitahidi leo Na mwendo utupasao, Mungu atatueleza Yatakayompendeza. 4. Mambo yetu ya dunia Mungu atayang’aria, Matata atageuza Yawe kwetu ya Baraka. 5. Yaliyo madogo, haya Mungu tukimfanyia, Yatosha: tutafaidi Huvuta kwake zaidi. 6. Ewe Bwana, siku zote, Tusaidie kwa yote: Mwendo wetu wote vivyo, Uwe kama tuombavyo.