Return to Index

11

12

Ewe Roho wa Mbinguni

13
SongInstrumental
	

1. Ewe Roho wa Mbinguni Uje kwetu sasa. Ufanye makazi yako Ndani ya Kanisa. 2. Ndiwe mwanga, umulike Tupate jikana; Mengi kwetu yapunguka, Tujalize, Bwana. 3. Ndiwe Moto, teketeza Taka zetu zote: Moyo na iwe sadaka Ya Mwokozi, yote. 4. Ndiwe Umande, na kwako Tutaburudika, Nchi kavu itakuwa Ni yenye Baraka. 5. Roho wa Mbinguni uwe Nasi hapa chini, Mwili uufananishe Na kichwa Mbinguni.*