Return to Index

120

121

Liko lango moja wazi

122
SongInstrumental
	

1. Liko lango moja wazi, Ni lango la mbinguni; Na wote waingiao Watapata nafasi. Lango ndiye Yesu Bwana Wote waingie kwake, Lango! Lango La Mbinguni ni wazi. 2. Yesu ndiye lango hili, Hata sasa ni wazi, Kwa wakubwa na wadogo, Tajiri na maskini. 3. Hili ni lango la raha, Ni lango la rehema; Kila mtu apitaye Hana majonzi tena. 4. Tukipita lango hili Tutatua mizigo, Tuliochukua kwanza, Tutavikwa uzima. 5. Hima ndugu tuingie Lango halijafungwa, Likifungwa mara moja Halitafunguliwa.