Return to Index

119

120

Enyi wanadamu mbona

121
SongInstrumental
	

1. Enyi wanadamu mbona Sana mwatanga-tanga, Kama kondoo wanyonge, Wasio na mchunga? Yuko mchunga mmoja Mwenye mapenzi mema; Haya kutaneni kwake, Atawachunga vyema. 2. Mungu tunamwona kuwa Mwenye uwezo wote; Na nguvu zake zapita Mawazo yetu yote: Ni Baba,mapenzi yake Ni makubwa hakika; Hatuwezi kuyajua, Na hayana mpaka. 3. Rehema za Mungu nazo Zina upana sana; Kama huo wa bahari, Mwisho wake hapana; Haki yake ina mema, Kwa hayo twashukuru, Kwetu uko msamaha, Furaha na uhuru. 4. Mapenzi yake mapana, Sisi hatuna cheo Cha kutosha, nao moyo Una wema upeo; Ukombozi mwingi mno Katika damu yake; Sote twapata furaha, Kwa maumivu yake. 5. Yesu mkaribieni Njoni msife myoyo; Njoni kwake kwa imani, Mema yake ni hayo; Heri tuwe kama wana Tushike neno lake, Daima atujaza Tele furaha yake.