Return to Index

125

126

Ni mji mzuri

127
SongInstrumental
	

1. Ni mji mzuri, Mbali sana; Watu wanawiri Kama jua; Waimba kwa tamu, Tuna wema hakimu: Sifa na idumu, Kwake Bwana. 2. Ni mji mzuri Twende sote! Una na fahari Msikawe! Raha tutaona, Dhambi hapana tena; Hatutaachana Siku zote. 3. Ni mji mzuri; Macho yote Huko wanawiri Kama pete; Baba tutamwona, Tukifanywa tu wana; Tumo kupendana Naye sote. 4. Ni mji mzuri; Tusipotee Na tuwe hodari, Tuupate! Tufunze, tutume Kwa taji na ufalme: Sifa na zivume Siku zote.