Return to Index

124

125

Ati twonane mtoni?

126
SongInstrumental
	

1. Ati twonane mtoni? Maji mazuri ya Mbingu; Yanatokea mwangani, Penye kiti cha Mungu. Naam, twonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni! Tutakutanika mtoni Penye kiti cha Mungu. 2. Tukitembea mtoni Na Yesu mchunga wetu Daima tu ibadani Usoni pake kwetu. 3. Kwang’ara sana mtoni Cha Mwokozi ni kioo, Milele hatuachani, Tumsifu kwa nyimbo. 4. Si mbali sana mtoni, Karibu tutawasili, Mara huwa furahani Na amani ya kweli.