Return to Index

123

124

Mungu ulisema

125
SongInstrumental
	

1. Mungu ulisema, Giza ilikoma; Twakushukuru! Twakusihi sote, Duniani mote Na kwa watu wote, Iwe nuru. 2. Yesu ulikuja, Ulituletea Nuru kuu; Macho kwa vipofu, Maisha kwa wafu; Twakushukuru. 3. Roho kiongozi, Roho wa mapenzi Tia nuru; Mwovu hata sasa Watu huwatosa, Tunakwomba hasa, Iwe nuru. 4. Mungu wa utatu Mwanga wao watu, Tuwe huru; Twende kote-kote Wafundishwe wote, Duniani mote, Iwe nuru.