Return to Index

133

134

Juu yake langu shaka

135
SongInstrumental
	

1. Juu yake langu shaka, Yesu namuwekea, Nami sitafedheheka Nikimtegemea. Natumai, natumai, Nnatumai kwake tu; Natumai, natumai, Natumai kwake tu. 2. Juu yake, dhambi zangu; Aniosha kwa damu; Nionekane kwa Mungu, Nisiye na laumu. 3. Juu yake yangu hofu; Kwake nimetulia; Sipotei kwa upofu Njia aning’azia. 4. Juu yake raha yangu; Humuangalia tu; Mwenye kila ulimwengu, Aniruzuku na huu. 5. Juu yake, moyo wangu; Hali yangu na mali; Mimi wake, Yeye wangu, Twapasana kamili.