Return to Index

136

137

Yesu ndiye mganga wetu

138
SongInstrumental
	

1. Yesu ndiye mganga wetu Aponya wagonjwa wote; Mganga wetu ni Yesu, Aponyaye hasira. Tumsifu huyo Yesu Tumsifu milele, Kwani Mponya mtakata Mwokozi wa wanyonge 2. Mganga wetu ni Yesu Huondoa matusi; Mganga wetu ni Yesu, Mwenye kuponya choyo. 3. Mganga wetu ni Yesu Huponya wivu wetu; Yesu ndiye aponyae Kelele za nyumbani. 4. Mganga wetu ni Yesu Mponya wa tamaa mbaya; Mganga wetu ni Yesu Uasherati hufuta 5. Mganga wetu ni Yesu Aponya kiu cha pombe, Mganga wetu ni Yesu Kila dhambi uponya