Return to Index

13

14

Yesu kwa imani

15
SongInstrumental
	

1. Yesu kwa imani, Nakutumaini, Peke yako; Nisikie sasa, Na kunitakasa, Ni wako kabisa Tangu leo. 2. Nipe nguvu pia Za kusaidia Moyo wangu; Ulikufa wewe, Wokovu nipewe Nakupenda wewe, Bwana wangu. 3. Hapa nazunguka Katika mashaka, Na matata; Palipo na giza Utaniongoza Hivi nitaweza Kufuata. 4. Takuwa mzima Nivushe salama Mautini; Sina hofu kamwe Ukiwapo nami Nami nikwandame Siku zote.*