Return to Index

14

15

Chakutumaini sina

16
SongInstrumental
	

1. Chakutumaini sina Ila damu yake Bwana, Sina wema wa kutosha Dhambi zangu kuziosha; Kwake Yesu nasimama, Ndiye mwamba: ni salama Ndiye mwamba: ni salama. 2. Njia yangu iwe ndefu Yeye hunipa wokovu; Mawimbi yakinipiga Nguvu zake ndiyo nanga. 3. Damu yake na sadaka Nategemea daima, Yote chini yakiisha Mwokozi atanitosha. 4. Nikiitwa hukumuni, Rohoni nina amani Nikivikwa haki yake Sina hofu mbele zake.