Return to Index

155

156

Bwana Yesu yuko wapi

157
SongInstrumental
	

1. Bwana Yesu yuko wapi, Mpenzi wangu rafiki? Njia gani amekwenda? Nitamwonaje mimi? Roho yangu yajutishwa Na dhambi na huzuni; Yesu mpenzi wangu Mwema Namtafuta kwa bidii. 2. Ninapaza sauti yangu Nalia:wapi Yesu? Ndani mwangu sina raha Mpaka nimwone Yesu. Ningekuwa na mabawa Ningeruka upesi Milimani, mabondeni Kumtafuta Bwanangu 3. Aondoa shida zangu, Maharibifu yote. Nikiona taabu mimi Anituliza yeye. Nitafanya bidii sana; Kumtafuta popote; Sitachoka kutembea Mchana hata usiku. 4. Bwana Yesu nitokee, Roho inakuita. Niondoe na maovu Yesu mwokozi wangu. Utilize hamu yangu Kaa kwangu daima. Nikupende sana wewe, Niwe wako milele.