Return to Index

17

18

Akifa Yesu nikafa naye

19
SongInstrumental
	

1. Akifa Yesu nikafa naye Uzima upya huishi naye; Humtazama mpaka nje: Nyakati zote ni wake yeye. Nyakati zote nimo pendoni, Nyakati zote ni uzimani, Humtazama hata atokee, Nyakati zote mimi ni wake. 2. Vita sipigi visivyo haki, Na Bwana wangu hapiganiki; Beramu yake haitwaliki, Napo po pote hila sitaki. 3. Sina mashaka, akawa mbali; Mizigo yote aihimili; Ananituliza Imanweli, Nyakati zote mimi husali. 4. Sina huzuni na mimi sidhii; Simwagi chozi, wala siguni; Sikuti afa, ila kitini Daima hunifikiri mimi. 5. Kila unyonge huusikia; Kila ugonjwa kwake hupoa; Yesu ni mwenye kuniokoa Nyakati zote hunijalia.