Return to Index

16

17

Namwndama Bwana kwa alilonena

18
SongInstrumental
	

1. Namwndama Bwana kwa alilonena Njia yangu huning’azia; Nikimridhisha atanidumisha Taamini nitii pia. Amini utii, njia pweke ni hii Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii. 2. Giza sina kwangu wala hata wingu Yeye mara huviondoa Woga, wasiwasi, sononeko, basi; Huamini nitii pia. 3. Masumbuko yote, sikitiko lote; Kwa mapenzi hunilipia; Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki Taamini nitii pia. 4. Mimi sitajua raha sawasawa Ila yote Yesu kumpa; Napata fadhili na radhi kamili, Taamini nitii pia. 5. Nitamfurahia na kumtumaini, Majumbani na njia-njia; Agizo natenda, nikitumwa hwenda, Huamini nitii pia.*