Return to Index

24

25

Nimekombolewa na Yesu

26
SongInstrumental
	

1. Nimekombolewa na Yesu Aliyenirehemia; Kwa bei ya mauti yake Nimekuwa mtoto wake. Kombolewa! Nakombolewa na damu; Kombolewa! Mimi mwana wake kweli. 2. Kukombolewa nafurahi, Kupita lugha kutamka; Kulionyesha pendo lake, Nimekuwa mtoto wake. 3. Nitamwona uzuri wake, Mfalme wangu wa ajabu; Na sasa najifurahisha, Katika neema yake. 4. Najua taji imewekwa Mbinguni tayari kwangu; Muda kitambo atakuja, Ili alipo, niwepo.