Return to Index

25

26

Yesu unipendaye

27
SongInstrumental
	

1. Yesu unipendaye Kwako nakimbilia, Ni wewe utoshaye, Mwovu akinijia; Yafiche ubavuni, Mwako maisha yangu; Nifiikishe mbinguni Wokoe moyo wangu. 2. Ngome nyingine sina; Nategemea kwako. Usinitupe Bwana , Nipe neema yako, Ninakuamania Mwenye kuniwezesha; Shari wanikingia, Vitani wanitosha. 3. Nakutaka Mpaji Vyote napata kwako; Niwapo muhitaji, Utanijazi vyako; Nao waangukao Wanyonge wape nguvu; Poza wauguao, Uongoze vipofu. 4. Bwana umeniosha Moyo kwa damu yako; Neema ya kutosha Yapatikana kwako; Kwako Bwana naona Kisima cha uzima; Mwangu moyoni Bwana, Bubujika daima.