Return to Index

33

34

Njoni! Njoni! Wenye dhambi

35
SongInstrumental
	

1. Njoni! Njoni! Wenye dhambi, Njoni, msikawie; Yesu awangojea ndiye awapendaye; Ajuaye awezaye kuwaponya ni Yeye. 2. Ewe muhitaji uje; Anakukaribisha, Imani, kweli, na toba, Neema ya kutosha, Jua sana, kwake Bwana Bure utapata. 3. Njoni, mliolemewa Na dhambi ya Adamu; Mkingoja kujiponya Mtapotea mumu; Si wa haki, ni wakosa Waoshwao kwa damu. 4. Ikamtokea dhiki, Mle Gethisemani; Kisha alipoangikwa Akalia mtini; ” Imekwisha”, alitosha Dhabihu ya thamani. 5. Kristo aliye Mbinguni Hutuombea huko; Basi mtumai yeye; Kamwe mwingine hako Yesu pweke, Yesu pweke, Ndiye Mwokozi wako. 6. Wamsifu-sifu sana Mbinguni malaika; Wachanganya nyimbo zao Na waliookoka: Aleluya wataimba Waliooshwa taka.