Return to Index

45

46

Twae wangu uzima

47
SongInstrumental
	

1. Twae wangu uzima, Sadaka ya daima; Twae saa na siku, Zikutukuze huku. 2. Twae mikono nayo Ifanye upendavyo, Twae yangu miguu Kwa wongozi wako tu. 3. Twae sauti yangu, Niimbe kwa Mungu tu; Itwae na midomo, Ijae neno lako. 4. Twae dhahabu pia, Na yote ya dunia; Twae yangu hekima, Upendavyo tumia. 5. Nia itwae, Mungu, Haitakuwa yangu; Twae moyo; ni wako, Uwe makazi yako. 6. Twae mapenzi yangu, Sifa za moyo wangu; Twae kabisa nafsi Niwe wako halisi.