Return to Index

46

47

Ni wako wewe nimekujua

48
SongInstrumental
	

1. Ni wako wewe, nimekujua, Na umeniambia; Lakini Bwana, nataka kwako nizidi kusongea. Bwana vuta, vuta, nije nisongee, Sana, kwako mtini. Bwana vuta, vuta, nije nisongee, Pa damu ya thamani. 2. Niweke sasa nikatumike Kwa nguvu za neema; Uyapendayo nami nipende, Nizidi kukwandama. 3. Nina furaha tele kila saa Nizungumzavyo kwako, Nikuombapo nami napata kujua nia yako. 4. Mapenzi yako hayapimiki, Ila ng’ambo ya liko. Anasa pia sitazijua, Bila kufika kwako.