Return to Index

47

48

Naweka dhambi zangu

49
SongInstrumental
	

1. Naweka dhambi zangu Juu yake Bwana Kuziondoa, kwangu Hulemea sana; Na uaili wangu Ameuondoa; Dawa yangu ni damu, Kwa hiyo napoa. 2. Na uhitaji wangu Nitamjuvisha Kwa upungufu wangu Yeye anatosha; Majonzi yangu yote Na mizigo yangu, Atachukua vyote Yesu Bwana wangu. 3. Na roho yangu nayo, Imechoka sana; Namletea hiyo Ilindwe na Bwana; Ni jema jina lake, Nalo lapendeza, Imanweli na kwake tutalitukuza. 4. Natamani daima Niwe kama Bwana, Mpole, tena mwema, Wa mapenzi sana; Zaidi natamani Kwenda kwake juu, Nikaone mbinguni Enzi yake kuu.