Return to Index

48

49

Nitwae hivi nilivyo

50
SongInstrumental
	

1. Nitwae hivi nilivyo, Umemwaga damu yako, Nawe ulivyoniita, Bwana Yesu,naja,naja. 2. Hivi nilivyo;si langu Kujiosha roho yangu; Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu,naja,naja. 3. Hivi nilivyo; sioni Kamwe furaha moyoni; Daima ni mashakani, Bwana Yesu,naja,naja. 4. Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu; Wewe u mtimilifu; Bwana Yesu,naja,naja. 5. Nawe hivi utanitwaa; Nisithubutu kukawa, Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu,naja,naja. 6. Hivi nilivyo;mapenzi Yamenipa njia wazi; Hali na mali sisazi, Bwana Yesu,naja,naja.