Return to Index

49

50

Yesu nakupenda U mali yangu

51
SongInstrumental
	

1. Yesu nakupenda, U mali yangu, Anasa za dhambi sitaki kwangu; Na Mwokozi aliyeniokoa, Sasa nakupenda, kuzidi pia. 2. Moyo umejaa mapenzi tele Kwa vile ulivyonipenda mbele, Uhai wako ukanitolea Sasa nakupenda, kuzidi pia. 3. Ulipoangikwa Msalabani Tusamehewe tulio dhambini; Taji ya miiba uliyoivaa, Sasa nakupenda, kuzidi pia. 4. Niwapo hai, niwapo maiti, Kupendana nawe kamwe siachi; Hari za kifo zikinienea, Sasa nakupenda, kuzidi pia. 5. Mawanda mazuri, na masikani Niyatazamapo huko Mbinguni, Tasema na taji nitakayovaa Sasa nakupenda, kuzidi pia.