Return to Index

54

55

Nipe moyo wenye sifa

56
SongInstrumental
	

1. Nipe moyo wenye sifa Sio wa utumwa; Moyo ulionyunyizwa Damu ya thamani. 2. Moyo msikizi, moyo Wa kunyenyekea, Moyo utawaliwao Na Mwokozi pia. 3. Mwenye kutubu, mnyonge, Sadiki, amini; Kamwe, kamwe asitengwe Akaaye ndani. 4. Mpya, mwema na mawazo Mwingi wa mapenzi Nawe uwe kielelezo Moyo wa Mwokozi. 5. Ni uule moyo wako; Moyo wa huruma Yesu, natamani kwako Kukujua vyema. 6. Na ya midomo matunda Yako, nipe nami; Amani isiyokoma Iwe yangu mimi. 7. Nitie yako tabia, Inishukie juu; Jina lako nipe pia, Ndilo la upendo. 8. Ni wa baba utukufu; Mwana atukuke; Na roho Mtakatifu U utatu pweke.