Return to Index

55

56

Ni siku kuu siku ile

57
SongInstrumental
	

1. Ni siku kuu siku ile Ya kumkiri Mwokozi! Moyo umejaa tele, Kunyamaza hauwezi. Siku kuu! Siku kuu! Ya kuoshwa dambi zangu kuu! Hukesha na kuomba tu, Ananiongoza miguu. Siku kuu! siku kuu! Ya kuoshwa dhambi zangu kuu. 2. Tumekwisha kupatana Mimi wake, yeye wangu, Na sasa nitamwandama, Nikiri neno la Mungu. 3. Moyo tulia kwa Bwana Kiini cha raha yako, Huna njia mbili tena; Yesu ndiye njia yako. 4. Nadhiri yangu ya mbele Nitaiweka daima, Hata ije siku ile, Ya kwonana kwa salama