Return to Index

57

58

Mwamba wenye imara

59
SongInstrumental
	

1. Mwamba wenye imara Kwako nitajificha! Maji hayo na damu Yaliyotoka humu, Hunisafi na dhambi, Hunifanya mshindi. 2. Kwa kazi zote pia , Sitimizi sharia. Nijapofanya bidii, Nikilia nakudhii, Hayaishi makosa; Ndiwe wa kuokoa. 3. Sina cha mkononi, Naja Msalabani; Nili tupu, nivike; Ni mnyonge, nishike; Nili mchafu naja, Nioshe nisijafa. 4. Nikungojapo chini, Nakwenda kaburini; Nipaapo Mbinguni, Na kukwona enzini: Roho yangu na iwe Rahani mwako wewe.