Return to Index

64

65

Katika safari yetu

66
SongInstrumental
	

1. Katika safari yetu Kwenda Mbinguni Tusiishe siku zetu Usingizini. Ng’oani! Tujifungeni, Twende zetu juu! Kristo ndiye kiongozi; Tusihofu tu. 2. Atwekwe badala yetu, Mwenyewe Bwana; Yesu kiongozi wetu Atapokea. 3. Kisimani, maji tele, Maji mazima! Maji hayo, Ya milele Yana neema. 4. Njiani miiba mingi, Yatuumiza; Hofu na hatari nyingi, Sana zakaza. 5. Kweli, njia ya Mbinguni Ni ya mashaka; Tuwe na Yesu njiani, Mara hufika.