Return to Index

73

74

Wachunga walipolinda

75
SongInstrumental
	

1. Wachunga walipolinda Kucha nyama zao, Malaika mtukufu Alishuka kwao. 2. Wakacha sana wachunga, Akawatuliza, “Nawaletea habari Ya kuwapendeza.” 3. ”Mji ule wa Daudi Leo amezawa Mwokozi ni Kristo Bwana, Ilivyoandikwa”. 4. ”Huyo mwana wa Mbinguni Ataonekana, Amelazwa kihorini Malazi hapana.” 5. Alipokwisha yanena Malaika hao Waliimba wimbo huu Usio na mwisho: 6. ”Enzi ni yake Munju juu, Na nchi salama, Kwa watu nao radhi kuu, Sasa na daima.”