Return to Index

80

81

Chini ya msalaba

82
SongInstrumental
	

1. Chini ya msalaba Nataka simama; Ndio mwamba safarini, Wa kivuli chema; Ni kweli kwa roho yangu Ni tuo kamili, Tatua mzigo wangu Wakati wa hari. 2. Hapa ni pema sana, Ni ngome kamili; Hapa yameonekana, Mapenzi ya kweli; Kama alivyoonyeshwa Yakobo zamani, Msalaba umekuwa Ngazi ya Mbinguni. 3. Na Yesu msalabani Walimkemea, Alikufa niokoke Niliyepotea; Naona ajabu sana Ya mambo mawili Jinsi alivyonipenda, Nisiyestahili. 4. Atakayeonana, Na Yesu Mbinguni, Njia yake aanzapo Ni msalabani; Wokovu upo hapa tu, Mwingine hapana, Kisha kuna furaha kuu Pamoja na Bwana.