Return to Index

88

89

Muda mwingi nilipotea

90
SongInstrumental
	

1. Muda mwingi nilipotea, Sikufahamu msalaba, Wala aliyenifilia, Kwa Kalvari. Rehema bure na neema, Samaha nalo nilipewa, Ndipo aliponifungua Kwa Kalvari. 2. Kwa neno lake Bwana Mungu, Nilijiona mimi mwovu, Nikageuka na kutubu, Kwa Kalvari. 3. Yote kwa Yesu namtolea, Ndiye mfalme wa pekee sasa, Kwa furaha nitamwimbia, Wa Kalvari. 4. Jinsi pendo lilivyo kuu, Neema ilishushwa toka juu, Alitufanyia wokovu Kwa Kalvari.