Return to Index

8

9

Yesu kwetu ni rafiki

10
SongInstrumental
	

1. Yesu kwetu ni rafiki, Hwambiwa haja pia; Tukiomba kwa Babaye Maombi asikia; Lakini twajikosesha, Twajitweka vibaya; Kwamba tulimwomba Mungu Dua angesikia. 2. Una dhiki na maonjo? Una mashaka pia. Haifai kufa moyo, Dua atasikia Hakuna mwingine mwema Wa kutuhurumia; Atujua tu dhaifu; Maombi asikia. 3. Je, hunayo hata nguvu, Huwezi kuendelea, Ujapodharauliwa Ujaporushwa pia, Watu wange kudharau, Wapendao dunia, Hukwambata mikononi, Dua atasikia.