Return to Index

7

8

Taji mvikeni

9
SongInstrumental
	

1. Taji mvikeni, Taji nyingi tena, Kondoo mwake kitini, Bwana wa mabwana; Nami tamsifu Alikufa kwangu, Ni mfalme mtukufu, Mkuu wa Mbingu. 2. Taji mvikeni Mwana wa bikira; Anazovaa kichwani Aliteka nyara; Shiloh wa wanabii, Mchunga wa watu, Shina na tanzu vya Yese, Wa Bethilehemu. 3. Taji mvikeni Bwana wa mapenzi; Jeraha zake ni shani Ni vito vya enzi, Mbinguni hakuna Hata malaika Awezaye kuziona Pasipo kushangaa.