Return to Index

96

97

Tazameni huyo ndiye

98
SongInstrumental
	

1. Tazameni huyo ndiye, Mwenye kushinda vita; Haya, tumsujudie; Nyara anazileta; Watu wote msifuni, Sasa yumo kitini. 2. Msifuni malaika, Mtukuzeni sana, Wote waliookoka Watamsifu Bwana; Watu wote msifuni, Sasa yumo kitini. 3. Walimfanya dhihaka Zamani wenye shari, Kwao waliookoka Ni Bwana wa fahari; Watu wote msifuni. Sasa yumo Kitini. 4. Nyimbo nzuri, sikizeni, Ni nyimbo za sifa kuu, Za Bwana Yesu kitini, Kutawazwa, yeye tu; Watu wote msifuni Sasa yumo Kitini.