Return to Index

113

114

Bwana Mungu nashangaa kabisa

115
SongInstrumental
	

1. Bwana Mungu, nashangaa kabisa Nikitazama kama vilivyo Nyota, ngurumo, vitu vingi vyote viumbwavyo kwa uwezo wako. Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu, Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu. 2. Nikitembea pote duniani, Ndege huimba, nawasikia, Milima hupendeza macho sana, Upepo nao nafurahia. 3. Nikikumbuka kama Wewe Mungu Ulivyompeleka Mwanao, Afe azichukue dhambi zetu, Kuyatambua ni vigumu mno. 4. Yesu Mwokozi utakaporudi Kunichukua kwenda Mbinguni, Nitashukuru na kwimba milele, Wote wajue jinsi ulivyo.