Return to Index

116

117

Tufani inapovuma

118
SongInstrumental
	

1. Tufani inapovuma Sana moyoni mwangu, Huona pa kujificha Mkononi mwa Mungu. Hunificha, hunificha Adui hatanipata, Hunificha, hunificha, Mkononi mwake. 2. Pengine kuna taabu Yanisongeza kwake; Naijua si hasira, Ni ya mapenzi yake. 3. Adui wakiniudhi Nami nikisumbuka, Mungu atavigeuza Vyote viwe baraka. 4. Niishipo duniani Ni tufani daima, Anilindapo rohoni Nitakaa salama.