Return to Index

144

145

Ndoa yetu nzima

146
SongInstrumental
	

1. Ndoa yetu nzima simika, Yesu! Usiku na mchana uwepo kwetu. Leo tuna raha, Wewe watupa. Ndoa yetu Bwana ndiwe Baraka! 2. Atoka kijana, ataka mchumba siku zinapita za kupimana. Leo twapatana pamoja kukaa Ndoa yetu… 3. Vyote hapa chini vinakaa muda, vyote vinaoza, tena vyachakaa. Pendo la duniani nalo huchakaa Ndoa yetu… 4. Kakaa kwetu Bwana, kutukagua, pendo letu sisi lisichakae: Hivi na tukae na baraka tu. Ndoa yetu… 5. Kana arusuni ulialikwa, walivyoishiwa ukaongeza, nasi shida zetu utazishinda. Ndoa yetu..