Return to Index

146

147

Tegemea mpaka kufa

148
SongInstrumental
	

1. Tegemea mpaka kufa, Utapata wokovu. Bwana Yesu ni Mwokozi Yeye anakupenda. Uje kwake ‘sikawie’. Yeye akuokoa. Njoo upesi! Njoo upesi! Fika kwa Bwana Yesu. 2. Acha mambo ya dunia Yakuhangaishayo. Iko mali ya uzima Unaitiwaa hiyo. Mali hiyo ni uzima Utapewa na Bwana. Njoo upesi! … 3. Wakatae, waepuke Wanaokudanganya; Na wajinga, wakuponza, Wakupoteza wewe. Ila wewe ukatae Kuondoka kwa Yesu. Njoo upesi! … 4. Ukijua jambo hilo Usipolifuata Kosa hilo kubwa sana, Wapasiwa hukumu. Vumilia, jizuie Utapata uzima. Njoo upesi! … 5. Bwana Yesu amekwisha Kukutengenezea Kitu chema kwake Mungu, Ndiko unakokwenda. Kile kitu upendacho Kule utakipewa. Njoo upesi! …