Return to Index

147

148

Ondokeni! tunaitwa

149
SongInstrumental
	

1. Ondokeni! tunaitwa na walinzi wa juu mnarani Yerusalemu, amka wee! Ni usiku wa manane, yuaja Bwana wa arusi, wanawali wako wapi? Amkeni upesi! Kaziwasheni taa. Haleluya! Fuateni arusini kwenda kumpokea Bwana! 2. Sayuni anasikia, moyo waruka kwa furaha, yu macho anaondoka. Mponya wake anashuka mbinguni mwenye utukufu, aleta mwanga wa kweli, taji yake yaja na Mwana wa Mungu. Hosiana! Twafuata kwenye shangwe tukale karamu yake. 3. Waimbiwa nyimbo nzuri kwa misemo ya watu wote na ya malaika mbinguni. Tukifika mjini kwako kwenye milango ya malulu tutakuimbia nasi. Furaha kama hii haijasikiwa duniani. Nasi sasa tunaimba, tunakusifu, Ee Bwana.